Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi.
Yobu 33:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nyama ya mwili wake itakuwa laini kuliko ya mtoto; Huzirudia siku za ujana wake; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hapo mwili wake utaweza kuwa tena kama kijana, ataweza kurudia tena nguvu zake za ujana. Biblia Habari Njema - BHND Hapo mwili wake utaweza kuwa tena kama kijana, ataweza kurudia tena nguvu zake za ujana. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hapo mwili wake utaweza kuwa tena kama kijana, ataweza kurudia tena nguvu zake za ujana. Neno: Bibilia Takatifu ndipo nyama ya mwili wake hufanywa mpya kama ya mtoto; hurudishwa upya kama siku za ujana wake. Neno: Maandiko Matakatifu ndipo nyama ya mwili wake hufanywa mpya kama ya mtoto; hurudishwa upya kama siku za ujana wake. BIBLIA KISWAHILI Nyama ya mwili wake itakuwa laini kuliko ya mtoto; Huzirudia siku za ujana wake; |
Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi.
Yeye humwomba Mungu, naye akamtakabalia; Hata auone uso wake kwa furaha; Naye humrejeshea mtu haki yake.
Kisha baada ya mambo hayo Ayubu akaishi miaka mia moja na arubaini, naye akawaona wanawe, na wana wa wanawe, hadi kizazi cha nne.
Nami nitampa mashamba yake ya mizabibu toka huko, na bonde la Akori kuwa mlango wa tumaini; naye ataniitikia huko, kama siku zile za ujana wake, na kama siku ile alipopanda kutoka nchi ya Misri.
Musa alikuwa mtu wa miaka mia moja na ishirini alipokufa; jicho lake halikupofuka, wala nguvu za mwili wake hazikupunguka.