Yobu 32:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tazama, tumbo langu ni kama divai iliyozibwa; Kama viriba vipya liko karibu kupasuka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Moyo wangu umefurika kama divai iliyozibwa, kama kiriba cha divai mpya tayari kupasuka. Biblia Habari Njema - BHND Moyo wangu umefurika kama divai iliyozibwa, kama kiriba cha divai mpya tayari kupasuka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Moyo wangu umefurika kama divai iliyozibwa, kama kiriba cha divai mpya tayari kupasuka. Neno: Bibilia Takatifu ndani yangu niko kama chupa iliyojazwa divai, kama kiriba kipya cha divai kilicho karibu kupasuka. Neno: Maandiko Matakatifu ndani yangu niko kama chupa iliyojazwa divai, kama kiriba kipya cha divai kilicho tayari kupasuka. BIBLIA KISWAHILI Tazama, tumbo langu ni kama divai iliyozibwa; Kama viriba vipya liko karibu kupasuka. |
Nami nikisema, Sitamtaja, wala sitasema tena kwa jina lake; basi, ndipo moyoni mwangu kumekuwamo kama moto uwakao, uliofungwa ndani ya mifupa yangu, nami nimechoka kwa kustahimili, wala siwezi kujizuia.
Lakini nimejaa ghadhabu ya BWANA; nimechoka kwa kujizuia; imwageni juu ya watoto walio njiani, na juu ya kusanyiko la vijana pia; maana hata mume atatwaliwa pamoja na mkewe, mzee pamoja na yeye aliyetimiza siku zake.
Simba amekwisha kunguruma, ni nani asiyeogopa? Bwana MUNGU amenena, ni nani awezaye neno ila kutabiri?
Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; na kama wakitia, vile viriba hupasuka, divai ikamwagika, na viriba vikaharibika; bali hutia divai mpya katika viriba vipya, vikahifadhika vyote.