Naye Yeremia akamlilia Yosia; na waimbaji wote wanaume kwa wawanawake wakamtaja Yosia katika maombolezo yao, hadi leo; hata wakayafanya kuwa ada kwa Israeli; nayo, tazama, yameandikwa katika Maombolezo.
Yobu 3:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na waulaani hao waulaanio mchana, Hao walio tayari kumwamsha huyo Lewiathani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Walozi wa siku waulaani, watu stadi wa kuligutua dude Lewiyathani waulaani! Biblia Habari Njema - BHND Walozi wa siku waulaani, watu stadi wa kuligutua dude Lewiyathani waulaani! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Walozi wa siku waulaani, watu stadi wa kuligutua dude Lewiyathani waulaani! Neno: Bibilia Takatifu Wale wanaozilaani siku na wailaani hiyo siku, wale walio tayari kumwamsha Lewiathani. Neno: Maandiko Matakatifu Wale wazilaanio siku wailaani hiyo siku, wale walio tayari kumwamsha Lewiathani. BIBLIA KISWAHILI Na waulaani hao waulaanio mchana, Hao walio tayari kumwamsha huyo Lewiathani. |
Naye Yeremia akamlilia Yosia; na waimbaji wote wanaume kwa wawanawake wakamtaja Yosia katika maombolezo yao, hadi leo; hata wakayafanya kuwa ada kwa Israeli; nayo, tazama, yameandikwa katika Maombolezo.
Nyota za mapambazuko yake na ziwe giza; Na utafute mwanga lakini usiupate; Wala usiyaone mapambazuko;
Hapana aliye mkali hata akathubutu kumwamsha; Bali ni nani awezaye kusimama mbele yangu mimi?
Katika siku hiyo BWANA, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu Lewiathani, nyoka yule mwepesi, na Lewiathani, nyoka yule mwenye kuzongazonga; naye atamwua yule joka aliye baharini.
Kwa ajili ya hayo, asema BWANA, Mungu wa majeshi, aliye Bwana; Kutakuwako maombolezo katika njia kuu zote; nao watasema katika njia zote, Ole! Ole! Nao watamwita mkulima aje kuombolea, na hao walio hodari wa kulia waje kuomboleza.
Wakafika nyumbani kwa yule mkuu wa sinagogi, akaona ghasia, na watu wakilia, wakifanya maombolezo makuu.