Na ipotelee mbali ile siku niliyozaliwa mimi, Na ule usiku uliosema, Mtoto wa kiume ametungishwa mimba.
Yobu 3:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Siku hiyo na iwe giza; Mungu asiiangalie toka juu, Wala mwanga usiiangazie. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku hiyo na iwe giza! Mungu juu asijishughulishe nayo! Wala nuru yoyote isiiangaze! Biblia Habari Njema - BHND Siku hiyo na iwe giza! Mungu juu asijishughulishe nayo! Wala nuru yoyote isiiangaze! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku hiyo na iwe giza! Mungu juu asijishughulishe nayo! Wala nuru yoyote isiiangaze! Neno: Bibilia Takatifu Siku ile na iwe giza; Mungu juu na asiiangalie; nayo nuru isiiangazie. Neno: Maandiko Matakatifu Siku ile na iwe giza; Mungu juu na asiiangalie; nayo nuru isiiangazie. BIBLIA KISWAHILI Siku hiyo na iwe giza; Mungu asiiangalie toka juu, Wala mwanga usiiangazie. |
Na ipotelee mbali ile siku niliyozaliwa mimi, Na ule usiku uliosema, Mtoto wa kiume ametungishwa mimba.
Ishikwe na giza, giza tupu, kuwa yake; Wingu na likae juu yake; Chote kiifanyacho siku kuwa giza na kiitishe.
siku ya giza na huzuni, siku ya mawingu na giza kuu. Kama mapambazuko yakitandazwa juu ya milima, hao ni wakuu, tena wenye nguvu, mfano wao haukuwako kamwe, wala hautakuwako baada ya hao, hata katika miaka ya vizazi vingi.
Ole wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya BWANA; kwa nini kuitamani siku ya BWANA? Ni giza, wala si nuru.
Jua wala nyota hazikuonekana kwa muda wa siku nyingi, na tufani kuu ikatushika, basi tukakata tamaa ya kuokoka.
nayo ni nchi itunzwayo na BWANA, Mungu wako; macho ya BWANA Mungu wako, ya juu yake, tangu mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka.
Na huyo wa tano akalimimina bakuli lake juu ya kiti cha enzi cha yule mnyama; ufalme wake ukatiwa giza; wakatafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu,