Yobu 3:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mbona mimi sikufa wakati nikizaliwa? Mbona nisitoe roho hapo nilipotoka tumboni? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mbona sikufa nilipozaliwa, nikatoka tumboni na kutoweka? Biblia Habari Njema - BHND Mbona sikufa nilipozaliwa, nikatoka tumboni na kutoweka? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mbona sikufa nilipozaliwa, nikatoka tumboni na kutoweka? Neno: Bibilia Takatifu “Kwa nini sikuangamia wakati wa kuzaliwa? Kwa nini sikufa nilipokuwa ninatoka tumboni? Neno: Maandiko Matakatifu “Kwa nini sikuangamia wakati wa kuzaliwa? Kwa nini sikufa nilipokuwa ninatoka tumboni? BIBLIA KISWAHILI Mbona mimi sikufa wakati nikizaliwa? Mbona nisitoe roho hapo nilipotoka tumboni? |
Nimekutegemea Wewe tangu kuzaliwa, Ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu, Ninakusifu Wewe daima.
naam, zaidi ya hao wote nikamwita heri yeye asiyekuwako bado, ambaye hakuyaona mabaya yanayotendeka chini ya jua.
Mtu akizaa watoto mia moja, akaishi miaka mingi, hata siku za maisha yake zikiwa nyingi, lakini nafsi yake haikushiba mema; tena ikiwa, zaidi ya hayo, amekosa maziko; mimi nasema, Heri mimba iliyoharibika kuliko huyo;
Nisikilizeni, enyi wa nyumba ya Yakobo, ninyi mlio mabaki ya nyumba ya Israeli, mliochukuliwa nami tangu tumboni, mlioinuliwa tangu mimbani;
Ole wangu, mama yangu, kwa kuwa umenizaa mtu wa kuteta, na mtu wa kushindana na dunia yote! Mimi sikukopesha kwa riba, wala watu hawakunikopesha kwa riba; lakini kila mmoja wao hunilaani.
kwa sababu hakuniua nilipotoka tumboni, na hivyo mama yangu angekuwa kaburi langu, na mimba yake sikuzote nzito.