Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako.
Yobu 3:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Baada ya hayo Ayubu akafunua kinywa chake, na kuilaani siku yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hatimaye Yobu aliamua kuongea, akailaani siku aliyozaliwa. Biblia Habari Njema - BHND Hatimaye Yobu aliamua kuongea, akailaani siku aliyozaliwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hatimaye Yobu aliamua kuongea, akailaani siku aliyozaliwa. Neno: Bibilia Takatifu Baada ya jambo hili, Ayubu akafumbua kinywa chake na kuilaani siku ya kuzaliwa kwake. Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya jambo hili, Ayubu akafumbua kinywa chake na kuilaani siku ya kuzaliwa kwake. BIBLIA KISWAHILI Baada ya hayo Ayubu akafunua kinywa chake, na kuilaani siku yake. |
Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako.
Kisha wakaketi ardhini pamoja naye muda wa siku saba, mchana na usiku, wala hapana mmoja aliyenena naye neno lolote; kwa maana waliona ya kuwa mashaka yake aliyo nayo ni makuu mno.
Lakini sasa nyosha mkono wako, uuguse mfupa wake na nyama yake, naye atakukufuru mbele za uso wako.
Na ipotelee mbali ile siku niliyozaliwa mimi, Na ule usiku uliosema, Mtoto wa kiume ametungishwa mimba.
Ole wangu, mama yangu, kwa kuwa umenizaa mtu wa kuteta, na mtu wa kushindana na dunia yote! Mimi sikukopesha kwa riba, wala watu hawakunikopesha kwa riba; lakini kila mmoja wao hunilaani.