Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi.
Yobu 29:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wakati nilipotoka kwenda mjini, kupitia langoni, Nilipokitengeza kiti changu katika njia kuu, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nilipokutana na wazee langoni mwa mji na kuchukua nafasi yangu mkutanoni, Biblia Habari Njema - BHND Nilipokutana na wazee langoni mwa mji na kuchukua nafasi yangu mkutanoni, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nilipokutana na wazee langoni mwa mji na kuchukua nafasi yangu mkutanoni, Neno: Bibilia Takatifu “Wakati nilienda kwenye lango la mji na kuketi katika kiwanja, Neno: Maandiko Matakatifu “Wakati nilipokwenda kwenye lango la mji na kuketi katika kiwanja, BIBLIA KISWAHILI Wakati nilipotoka kwenda mjini, kupitia langoni, Nilipokitengeneza kiti changu katika njia kuu, |
Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi.
Hamori, na Shekemu mwanawe, wakaja langoni pa mji wao, wakasema na watu wa mji wao, wakinena,
Karibu na malango, mahali pa kuingia mjini, Mahali pa kuyaingilia malango anapiga kelele.
Basi, Ebedmeleki, Mkushi, towashi, aliyekuwa katika nyumba ya mfalme, aliposikia kwamba wamemtia Yeremia shimoni; na wakati huo mfalme alikuwa amekaa katika lango la Benyamini;
Haya ndiyo mtakayoyatenda; kila mtu na aseme ukweli na jirani yake; katika malango yenu toeni hukumu za kweli na ziletazo amani;
Weka waamuzi na maofisa katika malango yako yote akupayo BWANA, Mungu wako, kwa hesabu ya kabila zako; nao wawaamue watu kwa maamuzi ya haki.
ndipo babaye na mamaye na wamkamate, na kumpeleka kwa wazee wa mji wake, katika lango la mahali pake;
Na watu wote waliokuwapo langoni, na wale wazee, wakasema, Naam, sisi ni mashahidi. BWANA na amfanye mwanamke huyu aingiaye nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea, wale wawili walioijenga nyumba ya Israeli. Nawe ufanikiwe katika Efrata, na kuwa mashuhuri katika Bethlehemu.