Atafunga punda wake katika mzabibu, Na mwanapunda wake katika mzabibu mzuri. Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi yake kwa damu ya zabibu.
Yobu 29:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wakati hatua zangu zilipokuwa zikioshwa kwa siagi, Nalo jabali liliponimiminia mito ya mafuta! Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nyakati hizo niliogelea kwenye ufanisi, miamba ilinitiririshia vijito vya mafuta! Biblia Habari Njema - BHND Nyakati hizo niliogelea kwenye ufanisi, miamba ilinitiririshia vijito vya mafuta! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nyakati hizo niliogelea kwenye ufanisi, miamba ilinitiririshia vijito vya mafuta! Neno: Bibilia Takatifu wakati njia yangu ilikuwa imenyeshewa siagi, nao mwamba ukanimiminia vijito vya mafuta ya zeituni. Neno: Maandiko Matakatifu wakati njia yangu ilikuwa imenyweshewa siagi, nao mwamba ukanimiminia vijito vya mafuta ya zeituni. BIBLIA KISWAHILI Wakati hatua zangu zilipokuwa zikioshwa kwa siagi, Nalo jabali liliponimiminia mito ya mafuta! |
Atafunga punda wake katika mzabibu, Na mwanapunda wake katika mzabibu mzuri. Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi yake kwa damu ya zabibu.
Wakati Mwenyezi alipokuwa angali pamoja nami, Nao watoto wangu walipokuwa wakinizunguka;
Naam, ningewalisha kwa ngano iliyo bora zaidi, Ningewashibisha kwa asali itokayo mwambani.
Hivyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha; na mavazi yako yalikuwa ya kitani safi, na hariri, na kazi ya taraza; ulikula unga mzuri, na asali, na mafuta; nawe ulikuwa mzuri mno, ukafanikiwa hata kufikia hali ya kifalme.
Na Asheri akamnena, Na abarikiwe Asheri kwa watoto; Na akubaliwe katika nduguze, Na achovye mguu wake katika mafuta.