Yobu 28:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Havitatajwa fedhaluka wala bilauri; Naam, kima cha hekima chapita marijani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hekima ina thamani kuliko matumbawe na marijani, thamani yake yashinda thamani ya lulu. Biblia Habari Njema - BHND Hekima ina thamani kuliko matumbawe na marijani, thamani yake yashinda thamani ya lulu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hekima ina thamani kuliko matumbawe na marijani, thamani yake yashinda thamani ya lulu. Neno: Bibilia Takatifu Marijani na yaspi hazistahili kutajwa; thamani ya hekima ni zaidi ya akiki nyekundu. Neno: Maandiko Matakatifu Marijani na yaspi hazistahili kutajwa; thamani ya hekima ni zaidi ya akiki nyekundu. BIBLIA KISWAHILI Havitatajwa fedhaluka wala bilauri; Naam, kima cha hekima chapita marijani. |
Wakuu wake walikuwa safi kuliko theluji, Walikuwa weupe kuliko maziwa; Miili yao, walikuwa wekundu kuliko marijani, Na umbo lao kama yakuti samawi.
Shamu alikuwa mfanya biashara kwako, kwa sababu ya wingi wa kazi za mkono wako walifanya biashara kwa zumaridi, urujuani, kazi ya taraza, kitani safi, marijani na akiki, wapate vitu vyako vilivyouzwa.
Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.
Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.
bidhaa ya dhahabu, fedha, vito vyenye thamani, lulu, kitani nzuri, nguo ya rangi ya zambarau, hariri na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, kila chombo cha pembe, kila chombo cha mti wa thamani nyingi, cha shaba, cha chuma na cha marimari;
Na ile milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu.