Yobu 28:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mwanadamu hajui thamani yake, Wala haionekani katika nchi ya walio hai. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hakuna mtu ajuaye thamani ya hekima, wala hekima haipatikani nchini mwa walio hai. Biblia Habari Njema - BHND Hakuna mtu ajuaye thamani ya hekima, wala hekima haipatikani nchini mwa walio hai. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hakuna mtu ajuaye thamani ya hekima, wala hekima haipatikani nchini mwa walio hai. Neno: Bibilia Takatifu Mwanadamu hatambui thamani yake; haiwezi kupatikana katika nchi ya walio hai. Neno: Maandiko Matakatifu Mwanadamu hatambui thamani yake; haiwezi kupatikana katika nchi ya walio hai. BIBLIA KISWAHILI Mwanadamu hajui thamani yake, Wala haionekani katika nchi ya walio hai. |
Ni za kutamanika kuliko dhahabu, Kuliko wingi wa dhahabu safi. Nazo ni tamu kuliko asali, Kuliko sega la asali.
Lakini Mungu atakuharibu hata milele; Atakuondolea mbali; Atakunyakua hemani mwako; Atakung'oa katika nchi ya walio hai.
Nilisema, Sitamwona BWANA, yeye BWANA, katika nchi ya walio hai; Sitamwona mwanadamu tena pamoja na hao wakaao duniani.
Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake ni nani angeyajali? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.
Lakini mimi nilikuwa kama mwana-kondoo mpole, achukuliwaye kwenda kuchinjwa; wala sikujua ya kuwa wamefanya mashauri kinyume changu, wakisema, Na tuuharibu mti pamoja na matunda yake, na tumkatilie mbali atoke katika nchi ya walio hai, ili jina lake lisikumbukwe tena.
Elamu yuko huko, na watu wake umati wote, pande zote za kaburi lake; wote pia wameuawa, wameanguka kwa upanga, walioshuka wakiwa hawajatahiriwa hadi pande za chini ya nchi; ambao waliwatia watu hofu katika nchi ya walio hai, nao wamechukua aibu yao, pamoja nao washukao shimoni.