BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa kiumbe hai.
Yobu 27:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC (Kwa kuwa uhai wangu ungali mzima ndani yangu, Na Roho ya Mungu iko katika pua yangu;) Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Naapa kuwa kadiri ninavyoweza kupumua, roho ya Mungu ikiwa bado ndani yangu; Biblia Habari Njema - BHND Naapa kuwa kadiri ninavyoweza kupumua, roho ya Mungu ikiwa bado ndani yangu; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Naapa kuwa kadiri ninavyoweza kupumua, roho ya Mungu ikiwa bado ndani yangu; Neno: Bibilia Takatifu kwa muda wote nitakaokuwa na uhai ndani yangu, nayo pumzi ya Mungu ikiwa puani mwangu, Neno: Maandiko Matakatifu kwa muda wote nitakaokuwa na uhai ndani yangu, nayo pumzi ya Mungu ikiwa puani mwangu, BIBLIA KISWAHILI (Kwa kuwa uhai wangu ungali mzima ndani yangu, Na Roho ya Mungu iko katika pua yangu;) |
BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa kiumbe hai.
Mwacheni mwanadamu ambaye pumzi yake iko katika mianzi ya pua yake; kwa maana wanafaa kitu gani?
wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu chochote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.