Yobu 27:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hao watakaosalia kwake watakufa kwa maradhi mabaya, Wala wajane wake waliofiwa na waume hawataomboleza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wale watakaopona watakufa kwa maradhi mabaya, na wajane wao hawatawaombolezea. Biblia Habari Njema - BHND Wale watakaopona watakufa kwa maradhi mabaya, na wajane wao hawatawaombolezea. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wale watakaopona watakufa kwa maradhi mabaya, na wajane wao hawatawaombolezea. Neno: Bibilia Takatifu Tauni itawazika wale watakaonusurika miongoni mwao, nao wajane wao hawatawaombolezea. Neno: Maandiko Matakatifu Tauni itawazika wale watakaonusurika miongoni mwao, nao wajane wao hawatawaombolezea. BIBLIA KISWAHILI Hao watakaosalia kwake watakufa kwa maradhi mabaya, Wala wajane wake waliofiwa na waume hawataomboleza. |
Basi, BWANA asema hivi, kuhusu habari za Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda; Hawatamwombolezea, wakisema, Aa! Ndugu yangu; au, Aa! Dada yangu; wala hawatamlilia, wakisema, Aa! Bwana wangu; au, Aa! Utukufu wake.
Na vilemba vyenu vitakuwa juu ya vichwa vyenu, na viatu vyenu miguuni mwenu; hamtaomboleza wala kulia; lakini mtafifia katika maovu yenu, na kusikitika kila mtu pamoja na mwenziwe.