Naye Hamani akawasimulia habari za fahari ya mali zake, na wingi wa watoto wake, na pia mambo yote ambayo mfalme amemfanikisha kwayo, na jinsi alivyompandisha cheo juu ya wakuu na watumishi wa mfalme.
Yobu 27:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Watoto wake wakiongezeka ni kwa upanga; Na wazao wake hawatashiba chakula. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watoto wake hata wawe wengi watauawa kwa upanga; wazawa wake hawatakuwa na chakula cha kutosha. Biblia Habari Njema - BHND Watoto wake hata wawe wengi watauawa kwa upanga; wazawa wake hawatakuwa na chakula cha kutosha. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watoto wake hata wawe wengi watauawa kwa upanga; wazawa wake hawatakuwa na chakula cha kutosha. Neno: Bibilia Takatifu Hata watoto wake wawe wengi kiasi gani, fungu lao ni kuuawa kwa upanga; wazao wake hawatakuwa kamwe na chakula cha kuwatosha. Neno: Maandiko Matakatifu Hata kama watoto wake watakuwa wengi kiasi gani, fungu lao ni kuuawa kwa upanga; wazao wake hawatakuwa kamwe na chakula cha kuwatosha. BIBLIA KISWAHILI Watoto wake wakiongezeka ni kwa upanga; Na wazao wake hawatashiba chakula. |
Naye Hamani akawasimulia habari za fahari ya mali zake, na wingi wa watoto wake, na pia mambo yote ambayo mfalme amemfanikisha kwayo, na jinsi alivyompandisha cheo juu ya wakuu na watumishi wa mfalme.
Simba mzee huangamia kwa kukosa mawindo, Nao watoto wa simba jike wametawanyika mbalimbali.
Kwa maana tazama, siku zitakuja watakaposema, Heri walio tasa, na matumbo yasiyozaa, na maziwa yasiyonyonyesha.
Wanao na binti zako litapewa taifa lingine, na macho yako yataangalia, na kuzimia kwa kuwatamani mchana kutwa; wala hapatakuwa na kitu katika uwezo wa mkono wako.
Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula, Lakini waliokuwa na njaa sasa hawana njaa tena. Naam, huyo aliyekuwa tasa amezaa watoto saba, lakini aliye na watoto wengi amehuzunika.