Yobu 26:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Huyafunga maji ndani ya mawingu yake mazito; Na hilo wingu halipasuki chini yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema huyafunga maji mawinguni yawe mazito, nayo mawingu hayapasuki kwa uzito wake. Biblia Habari Njema - BHND huyafunga maji mawinguni yawe mazito, nayo mawingu hayapasuki kwa uzito wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza huyafunga maji mawinguni yawe mazito, nayo mawingu hayapasuki kwa uzito wake. Neno: Bibilia Takatifu Huyafungia maji kwenye mawingu yake, hata hivyo mawingu hayapasuki kwa uzito wake. Neno: Maandiko Matakatifu Huyafungia maji kwenye mawingu yake, hata hivyo mawingu hayapasuki kwa uzito wake. BIBLIA KISWAHILI Huyafunga maji ndani ya mawingu yake mazito; Na hilo wingu halipasuki chini yake. |
Ni nani awezaye kuyahesabu mawingu kwa hekima? Au ni nani awezaye kuzimimina chupa za mbinguni?
Ndiye apandishaye mvuke toka miisho ya nchi; Huifanyia mvua umeme; Hutoa upepo katika ghala zake.
Ni nani aliyepanda mbinguni na kushuka chini? Ni nani aliyekamata upepo kwa makonzi yake? Ni nani aliyeyafunga maji ndani ya nguo yake? Ni nani aliyefanya imara ncha zote za nchi? Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe, kama wajua?
nami nitaliharibu; wala halitapogolewa wala kulimwa, bali litamea mbigili na miiba; nami nitayaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake.
Atoapo sauti yake, pana mshindo wa maji mbinguni, Naye hupandisha mawingu toka ncha za nchi; Huifanyia mvua umeme, Huutoa upepo katika hazina zake.