Yobu 26:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi isiyo na kitu, Na kuutundika ulimwengu pasipo kitu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mungu hutandaza kaskazini mahali patupu, na hutundika dunia mahali pasipo na kitu, Biblia Habari Njema - BHND Mungu hutandaza kaskazini mahali patupu, na hutundika dunia mahali pasipo na kitu, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mungu hutandaza kaskazini mahali patupu, na hutundika dunia mahali pasipo na kitu, Neno: Bibilia Takatifu Hutandaza anga la kaskazini mahali patupu; naye huining’iniza dunia mahali pasipo na kitu. Neno: Maandiko Matakatifu Hutandaza anga la kaskazini mahali patupu; naye huining’iniza dunia mahali pasipo na kitu. BIBLIA KISWAHILI Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi isiyo na kitu, Na kuutundika ulimwengu pasipo kitu. |
Je! Hamkujua? Hamkusikia? Hamkuambiwa tokea mwanzo? Hamkufahamu tangu kuwekwa misingi ya dunia?
Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanaokaa ndani yake huwa kama panzi; yeye ndiye azitandazaye mbingu kama pazia na kuzikunjua kama hema ya kukaliwa;
Inueni macho yenu juu, mkaone; ni nani aliyeziumba hizi; aletaye nje jeshi lao kwa hesabu; aziita zote kwa majina; kwa ukuu wa uweza wake, na kwa kuwa yeye ni hodari kwa nguvu zake; hapana moja isiyokuwapo mahali pake.
Mungu BWANA anena, yeye aliyeziumba mbingu, na kuzitanda; yeye aliyeitandaza nchi na mazao yake; yeye awapaye pumzi watu walio juu yake; yeye awapaye roho wao waendao ndani yake.
Ufunuo wa neno la BWANA juu ya Israeli. Haya ndiyo asemayo BWANA, azitandaye mbingu, auwekaye msingi wa dunia, aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake.