Ni juu mno kama mbingu; waweza kufanya nini wewe? Ni wenye kina kuliko kuzimuni; waweza kujua nini wewe?
Yobu 26:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kaburi li wazi mbele yake, Uharibifu nao hauna kifuniko. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kuzimu kuko wazi kabisa mbele ya Mungu. Abadoni haina kifuniko chochote. Biblia Habari Njema - BHND Kuzimu kuko wazi kabisa mbele ya Mungu. Abadoni haina kifuniko chochote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kuzimu kuko wazi kabisa mbele ya Mungu. Abadoni haina kifuniko chochote. Neno: Bibilia Takatifu Mauti iko wazi mbele za Mungu; Uharibifu haukufunikwa. Neno: Maandiko Matakatifu Mauti iko wazi mbele za Mungu; Uharibifu haukufunikwa. BIBLIA KISWAHILI Kaburi li wazi mbele yake, Uharibifu nao hauna kifuniko. |
Ni juu mno kama mbingu; waweza kufanya nini wewe? Ni wenye kina kuliko kuzimuni; waweza kujua nini wewe?
Ni nani aliyetangulia kunipa hata nimlipe? Kila kilicho chini ya mbingu nzima ni changu.
Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili yako, Ili kukulaki utakapokuja; Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako, Naam, walio wakuu wote wa dunia; Huwainua wafalme wote wa mataifa, Watoke katika viti vyao vya enzi.
Wajapochimba waingie katika kuzimu, mkono wangu utawatoa huko; nao wajapopanda hata mbinguni, nitawateremsha toka huko.
Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, maana vitu vyote ni tupu na kuwekwa wazi machoni pake yeye ambaye tunapaswa kuwajibika kwake.
Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kigiriki analo jina lake Apolioni.