Yobu 26:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tazama, hivi ni viunga tu vya njia zake; Na jinsi yalivyo madogo manong'ono tusikiayo katika habari zake! Lakini ngurumo za uweza wake ni nani awezaye kuzielewa? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yamkini haya ni machache tu ya matendo yake, ni minongono tu tunayosikia juu yake. Nani awezaye kujua ukuu wa nguvu yake?” Biblia Habari Njema - BHND Yamkini haya ni machache tu ya matendo yake, ni minongono tu tunayosikia juu yake. Nani awezaye kujua ukuu wa nguvu yake?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yamkini haya ni machache tu ya matendo yake, ni minong'ono tu tunayosikia juu yake. Nani awezaye kujua ukuu wa nguvu yake?” Neno: Bibilia Takatifu Haya ni mambo madogo tu katika matendo yake; tazama jinsi ulivyo mdogo mnong’ono tunaousikia kumhusu! Ni nani basi awezaye kuelewa ngurumo za nguvu zake?” Neno: Maandiko Matakatifu Haya ni mambo madogo tu katika matendo yake; tazama jinsi ulivyo mdogo mnong’ono tunaousikia kumhusu! Ni nani basi awezaye kuelewa ngurumo za nguvu zake?” BIBLIA KISWAHILI Tazama, hivi ni viunga tu vya njia zake; Na jinsi yalivyo madogo manong'ono tusikiayo katika habari zake! Lakini ngurumo za uweza wake ni nani awezaye kuzielewa? |
Baadaye sauti hunguruma; Yeye hunguruma kwa sauti ya ukuu wake; Hazizuii hapo sauti yake isikiwapo.
Mungu hunguruma kwa kustaajabisha kwa sauti yake; Hufanya mambo makuu, ambayo hatuwezi kuyaelewa.
Nilikuwa nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio; Bali sasa jicho langu linakuona.
Sauti ya BWANA inasikika juu ya maji; Mungu wa utukufu apiga radi; BWANA yu juu ya maji mengi.
Kama vile wewe usipojua njia ya upepo ni ipi, wala jinsi mifupa ikuavyo tumboni mwake mja mzito; kadhalika huijui kazi ya Mungu, afanyaye mambo yote.
Mwangaza wake ulikuwa kama nuru; Alikuwa na mishale ya nuru ubavuni pake; Ndipo ulipofichwa uweza wake.
Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazieleweki!
Washindanao na BWANA watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; BWANA ataihukumu dunia yote; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake.