Yobu 26:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Huichafua bahari kwa uwezo wake, Na kumtema Rahabu kwa akili zake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa nguvu zake aliituliza bahari; kwa maarifa yake alimwangamiza dude Rahabu. Biblia Habari Njema - BHND Kwa nguvu zake aliituliza bahari; kwa maarifa yake alimwangamiza dude Rahabu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa nguvu zake aliituliza bahari; kwa maarifa yake alimwangamiza dude Rahabu. Neno: Bibilia Takatifu Kwa nguvu zake aliisukasuka bahari; kwa hekima yake alimkata Rahabu vipande vipande. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa nguvu zake aliisukasuka bahari; kwa hekima yake alimkata Rahabu vipande vipande. BIBLIA KISWAHILI Huichafua bahari kwa uwezo wake, Na kumtema Rahabu kwa akili zake. |
Kwa maana kutakuwa siku ya BWANA wa majeshi juu ya watu wote wenye kiburi na majivuno, na juu ya yote yaliyoinuka; nayo yatashushwa chini.
Amka, amka, jivike nguvu, Ee mkono wa Bwana; Amka kama katika siku zile za kale, Katika vizazi vile vya zamani.
BWANA asema hivi, awapaye watu jua, ili kuwa nuru wakati wa mchana, na amri za mwezi na nyota, ili kuwa nuru wakati wa usiku, aichafuaye bahari, hata mawimbi yake yakavuma; BWANA wa majeshi, ndilo jina lake;
Basi mimi, Nebukadneza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili.
Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.