Ndipo nchi ilipotikisika na kutetemeka, Misingi ya mbinguni ikasukasuka Na kutikisika, kwa sababu alikuwa na ghadhabu.
Yobu 26:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nguzo za mbingu zatetemeka, Na kustaajabu kwa kukemea kwake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mungu akitoa sauti ya kukemea, nguzo za mbingu hutetemeka na kustaajabu. Biblia Habari Njema - BHND Mungu akitoa sauti ya kukemea, nguzo za mbingu hutetemeka na kustaajabu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mungu akitoa sauti ya kukemea, nguzo za mbingu hutetemeka na kustaajabu. Neno: Bibilia Takatifu Nguzo za mbingu nazo zatetemeka, zinatishika anapozikemea. Neno: Maandiko Matakatifu Nguzo za mbingu nazo zatetemeka, zinatishika anapozikemea. BIBLIA KISWAHILI Nguzo za mbingu zatetemeka, Na kustaajabu kwa kukemea kwake. |
Ndipo nchi ilipotikisika na kutetemeka, Misingi ya mbinguni ikasukasuka Na kutikisika, kwa sababu alikuwa na ghadhabu.
Ndipo nchi iliyotikisika na kutetemeka, Misingi ya milima ikatingizika; Ikatikisika kwa sababu alikuwa na ghadhabu.
Milima hutetema mbele zake, navyo vilima huyeyuka; nayo dunia huinuliwa mbele za uso wake, naam, dunia na wote wakaao ndani yake.
Ni nani awezaye kusimama mbele za ghadhabu yake, naye ni nani awezaye kukaa katika ukali wa hasira yake? Hasira yake kali humwagwa kama moto, nayo majabali yapasuliwa na yeye.
Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwizi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.
Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.
Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina BWANA, Naye ameuweka ulimwengu juu yake.