Yobu 24:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Huwanyang'anya yatima punda wao, Humtwaa rehani ng'ombe wake mwanamke mjane. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huwanyanganya yatima punda wao, humweka rehani ng'ombe wa mjane. Biblia Habari Njema - BHND Huwanyanganya yatima punda wao, humweka rehani ng'ombe wa mjane. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huwanyang'anya yatima punda wao, humweka rehani ng'ombe wa mjane. Neno: Bibilia Takatifu Huwanyang’anya yatima punda wao, na kumchukua rehani fahali wa mjane. Neno: Maandiko Matakatifu Huwanyang’anya yatima punda wao, na kumchukua rehani fahali wa mjane. BIBLIA KISWAHILI Huwanyang'anya yatima punda wao, Humtwaa rehani ng'ombe wake mwanamke mjane. |
Ikiwa wewe kwa njia yoyote wapokea nguo ya jirani yako rehani, lazima utamrudishia mbele ya jua kuchwa;
Mtu awaye yote asitwae jiwe la kusagia, la juu wala la chini, kuwa rehani; kwani hivi ni kutwaa maisha ya mtu kuwa rehani.
Mtu akionekana anamwiba nduguze mmojawapo katika wana wa Israeli, akamfanya kama mtumwa, au kumwuza; na afe mwizi huyo; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.
Nami nipo hapa; basi, mnishuhudie mbele za BWANA, na mbele ya masihi wake, nilitwaa ng'ombe wa nani? Au nilitwaa punda wa nani? Au ni nani niliyemdhulumu? Ni nani niliyemwonea? Au kwa mkono wa nani nimepokea rushwa inipofushe macho? Nami nitawarudishia ninyi.