mara Waseba wakawashambulia, wakawachukua wakaenda nao; naam, wamewaua hao watumishi kwa makali ya upanga, mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.
Yobu 24:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wako waziondoao alama za mipaka; Huyachukua makundi na kuyalisha. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wanaoondoa alama za mipaka ya mashamba, na wengine huiba mifugo na kuilisha. Biblia Habari Njema - BHND Watu wanaoondoa alama za mipaka ya mashamba, na wengine huiba mifugo na kuilisha. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wanaoondoa alama za mipaka ya mashamba, na wengine huiba mifugo na kuilisha. Neno: Bibilia Takatifu Watu husogeza mawe ya mpaka; huchunga makundi ya wanyama waliyonyang’anya kwa nguvu. Neno: Maandiko Matakatifu Watu husogeza mawe ya mpaka; huchunga makundi ya wanyama waliyonyang’anya kwa nguvu. BIBLIA KISWAHILI Wako waziondoao alama za mipaka; Huyachukua makundi na kuyalisha. |
mara Waseba wakawashambulia, wakawachukua wakaenda nao; naam, wamewaua hao watumishi kwa makali ya upanga, mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.
Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wakaldayo walifanya vikosi vitatu, wakawaangukia ngamia, wakaenda nao, naam, wamewaua wale watumishi kwa makali ya upanga; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.
Kwa maana amewaonea na kuwaacha maskini; Amenyang'anya nyumba kwa jeuri, wala hataijenga.
Mavuno yake wale wenye njaa huyala, Na kuyatwaa hata kuyatoa miibani, Nao wenye kiu huzitwetea mali zao.
Wakuu wa Yuda ni kama watu waondoao alama ya mpaka; nitawamwagia ghadhabu yangu kama maji.
Usiiondoe alama ya mpaka wa jirani yako, waliouweka watu wa kale katika urithi wako, utakaorithi ndani ya nchi akupayo BWANA, Mungu wako, uimiliki.