Yobu 23:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hapo waelekevu wangepata kuhojiana naye; Basi hivyo ningeachiliwa na mwamuzi wangu milele. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yeye aweza kuzungumza na mtu mnyofu, Mungu, hakimu wangu angeamua kuwa sina hatia milele. Biblia Habari Njema - BHND Yeye aweza kuzungumza na mtu mnyofu, Mungu, hakimu wangu angeamua kuwa sina hatia milele. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yeye aweza kuzungumza na mtu mnyofu, Mungu, hakimu wangu angeamua kuwa sina hatia milele. Neno: Bibilia Takatifu Hapo mtu mwadilifu angeleta kesi yake mbele zake, nami ningeokolewa milele na mhukumu wangu. Neno: Maandiko Matakatifu Hapo mtu mwadilifu angeweka shauri lake mbele zake, nami ningeokolewa milele na mhukumu wangu. BIBLIA KISWAHILI Hapo wanyofu wangepata kuhojiana naye; Basi hivyo ningeachiliwa na mwamuzi wangu milele. |
Ambaye, nijapokuwa mimi ni mwenye haki, siwezi kumjibu; Ni lazima nimwombe mshitaki wangu anihurumie.
Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama damu, zitakuwa kama sufu.
Wewe u mwenye haki, Ee BWANA, nitetapo nawe, lakini nitasema nawe katika habari ya haki. Mbona njia ya wabaya inasitawi? Mbona wote watendao hila wanakaa salama?
Je! Ataishika hasira yake hata milele? Ataishika hata mwisho? Tazama, umesema hivyo, bali umetenda mambo mabaya, umefuata njia yako mwenyewe.