Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako itakuwa kubwa sana.
Yobu 22:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naye Mwenyezi atakuwa hazina yako, Atakuwa ni fedha ya thamani kwako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mungu Mwenye Nguvu akawa ndio dhahabu yako, na fedha yako ya thamani; Biblia Habari Njema - BHND Mungu Mwenye Nguvu akawa ndio dhahabu yako, na fedha yako ya thamani; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mungu Mwenye Nguvu akawa ndio dhahabu yako, na fedha yako ya thamani; Neno: Bibilia Takatifu ndipo Mwenyezi atakuwa dhahabu yako, naye atakuwa fedha yako iliyo bora. Neno: Maandiko Matakatifu ndipo Mwenyezi atakuwa dhahabu yako, naye atakuwa fedha yako iliyo bora. BIBLIA KISWAHILI Naye Mwenyezi atakuwa hazina yako, Atakuwa ni fedha ya thamani kwako. |
Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako itakuwa kubwa sana.
BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.
Kwa kuwa BWANA, Mungu, ni jua na ngao, BWANA atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu.
Nyakati zako zitakuwa nyakati za kukaa imara; za wokovu tele na hekima na maarifa; kumcha BWANA ni hazina yake ya akiba.
usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kulia wa haki yangu.
kama wenye huzuni, bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote.
Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?