Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Yobu 22:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Je! Yumkini mtu awaye yote kumfaa Mungu? Hakika yeye aliye na hekima hujifaa mwenyewe.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

“Je, binadamu anafaa chochote kwa Mungu? Kwa kweli mwenye hekima anajifaidi mwenyewe tu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

“Je, binadamu anafaa chochote kwa Mungu? Kwa kweli mwenye hekima anajifaidi mwenyewe tu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

“Je, binadamu anafaa chochote kwa Mungu? Kwa kweli mwenye hekima anajifaidi mwenyewe tu.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

“Je, mwanadamu aweza kuwa wa faida kwa Mungu? Je, hata mtu mwenye hekima aweza kumfaidi?

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

“Je, mwanadamu aweza kuwa wa faida kwa Mungu? Je, hata mtu mwenye hekima aweza kumfaidi?

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Je! Yamkini mtu awaye yote kumfaa Mungu? Hakika yeye aliye na hekima hujifaa mwenyewe.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Yobu 22:2
15 Marejeleo ya Msalaba  

Huyo Mwenyezi ni nani, hata tumtumikie? Nasi tutafaidiwa nini tukimwomba?


Ndipo huyo Elifazi Mtemani akajibu, na kusema,


Je! Mwenyezi hupata furaha katika wewe kuwa mwenye haki? Au je, ni faida kwake, kwamba wafanya njia zako kuwa timilifu?


Je! Mtu ni kitu gani, hata ukamtukuza, Na kumtia moyoni mwako,


Nimemwambia BWANA, Ndiwe BWANA wangu; Sina wema ila utokao kwako.


Kama una hekima, una hekima kwa nafsi yako; Na kama una dharau, utaichukua peke yako.


Jicho lako la kulia likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee kuliko mwili wako wote utupwe katika Jehanamu.


Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.


wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu chochote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.


kuzifuata amri za BWANA na sheria zake, ninazokuamuru leo, upate uheri?