Katika mwaka wa mia sita wa maisha ya Nuhu, mwezi wa pili, siku ya kumi na saba ya mwezi, siku ile chemchemi zote za vilindi vikuu zilibubujika kwa nguvu, madirisha ya mbinguni yakafunguka.
Yobu 22:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ambao walinyakuliwa kabla ya wakati wao, Msingi wao ulimwagika kama kijito cha maji; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hao walifagiliwa kabla ya wakati wao, misingi yao ilikumbwa mbali na maji. Biblia Habari Njema - BHND Hao walifagiliwa kabla ya wakati wao, misingi yao ilikumbwa mbali na maji. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hao walifagiliwa kabla ya wakati wao, misingi yao ilikumbwa mbali na maji. Neno: Bibilia Takatifu Waliondolewa kabla ya wakati wao, misingi yao ikachukuliwa na mafuriko. Neno: Maandiko Matakatifu Waliondolewa kabla ya wakati wao, misingi yao ikachukuliwa na mafuriko. BIBLIA KISWAHILI Ambao walinyakuliwa kabla ya wakati wao, Msingi wao ulimwagika kama kijito cha maji; |
Katika mwaka wa mia sita wa maisha ya Nuhu, mwezi wa pili, siku ya kumi na saba ya mwezi, siku ile chemchemi zote za vilindi vikuu zilibubujika kwa nguvu, madirisha ya mbinguni yakafunguka.
Maji mengi huyapunguza mawe; Mafuriko yake huuchukua mchanga wa nchi; Nawe matumaini ya wanadamu wayaangamiza.
Mwasema, Yeye ni mwepesi juu ya uso wa gharika; Sehemu yao inalaaniwa duniani; Hageuki kwenda njia ya mizabibuni.
Je! Si zaidi sana hao wakaao katika nyumba za udongo, Ambazo misingi yao i katika mchanga, Hao wanaopondwa kama nondo!
Nitasema, Ee Mungu wangu, usiniondoe katikati ya siku zangu; Miaka yako ni tangu kizazi hata kizazi.
Nawe, Ee Mungu, utawateremsha, Wafikie shimo la uharibifu; Watu wa damu na hila hawataishi nusu ya siku zao, Bali mimi nitakutumaini Wewe.
Tazama, Bwana ana mmoja aliye hodari, mwenye nguvu; kama dhoruba ya mvua ya mawe, tufani iharibuyo, kama dhoruba ya maji mengi yafurikayo, ndivyo atakavyotupa chini kwa mkono.
wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi Nuhu, mjumbe wa haki, na watu wengine saba, hapo alipoleta Gharika juu ya ulimwengu wa wasiomcha Mungu;