Yobu 22:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nawe wasema, Mungu anajua nini? Je! Aweza kuamua kati ya giza kuu? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini wewe wasema: ‘Mungu ajua nini? Je, aweza kupenya mawingu akatoa hukumu? Biblia Habari Njema - BHND Lakini wewe wasema: ‘Mungu ajua nini? Je, aweza kupenya mawingu akatoa hukumu? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini wewe wasema: ‘Mungu ajua nini? Je, aweza kupenya mawingu akatoa hukumu? Neno: Bibilia Takatifu Hivyo wewe wasema, ‘Mungu anajua nini?’ Je, yeye huhukumu katika giza kama hilo? Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo wewe wasema, ‘Mungu anajua nini?’ Je, yeye huhukumu katika giza kama hilo? BIBLIA KISWAHILI Nawe wasema, Mungu anajua nini? Je! Aweza kuamua kati ya giza kuu? |
Walijifanya hodari katika jambo baya; Hushauriana juu ya kutega mitego; Wakisema, Ni nani atakayeiona?
Ole wao wanaojitahidi kumficha BWANA mashauri yao, na matendo yao yamo gizani, nao husema, Ni nani atuonaye? Nani atujuaye?
Je, mtu yeyote aweza kujificha mahali pa siri, nisimwone? Asema BWANA. Je! Mbingu na nchi hazikujawa nami? Asema BWANA.
Kisha akaniambia, Mwanadamu, umeyaona wanayotenda wazee wa nyumba ya Israeli gizani, kila mtu ndani ya vyumba vyake vya sanamu? Maana husema, BWANA hatuoni; BWANA ameiacha nchi hii.
Ndipo akaniambia, Uovu wa nyumba ya Israeli na Yuda ni mwingi sana, nayo nchi imejaa damu, nao mji umejaa kupotosha hukumu; maana husema, BWANA ameiacha nchi hii, naye BWANA haoni.
Wajapochimba waingie katika kuzimu, mkono wangu utawatoa huko; nao wajapopanda hata mbinguni, nitawateremsha toka huko.
Nao wajapojificha katika kilele cha Karmeli, nitawatafuta na kuwatoa toka huko; na wajapositirika katika vilindi vya bahari nisiwaone, nitamwagiza joka huko, naye atawauma.
Kisha itakuwa wakati ule, nitauchunguza Yerusalemu kwa taa; nami nitawaadhibu watu walioganda juu ya masira yao; wasemao katika mioyo yao, BWANA hatatenda mema, wala hatatenda mabaya.