Yobu 22:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Au je! Huoni giza, Na maji mengi yanayokufunika? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Giza limekuangukia usione kitu; mafuriko ya maji yamekufunika. Biblia Habari Njema - BHND Giza limekuangukia usione kitu; mafuriko ya maji yamekufunika. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Giza limekuangukia usione kitu; mafuriko ya maji yamekufunika. Neno: Bibilia Takatifu ndiyo sababu ni giza sana huwezi kuona, tena ndiyo sababu mafuriko ya maji yamekufunika. Neno: Maandiko Matakatifu ndiyo sababu ni giza sana huwezi kuona, tena ndiyo sababu mafuriko ya maji yamekufunika. BIBLIA KISWAHILI Au je! Huoni giza, Na maji mengi yanayokufunika? |
Mwasema, Yeye ni mwepesi juu ya uso wa gharika; Sehemu yao inalaaniwa duniani; Hageuki kwenda njia ya mizabibuni.
Kilindi chapigia kelele kilindi kwa sauti ya maporomoko ya maji yako, Gharika zako zote na mawimbi yako yote yamepita juu yangu.
nao wataiangalia nchi, na, tazama, shida na giza; hapatakuwa changamko kwa sababu ya dhiki; nao watafukuzwa na kuingia katika giza kubwa.
Maana ulinitupa vilindini, Ndani ya moyo wa bahari; Gharika ya maji ikanizunguka pande zote; Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu.
bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.