Ikiwa nimeuita uharibifu, Wewe u baba yangu; Na kuliambia buu, Wewe u mama yangu, na dada yangu;
Yobu 21:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wao hulala mavumbini sawasawa, Mabuu huwafunika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hata hivyo, wote hufa na kuzikwa, wote hufunikwa na mabuu. Biblia Habari Njema - BHND Hata hivyo, wote hufa na kuzikwa, wote hufunikwa na mabuu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hata hivyo, wote hufa na kuzikwa, wote hufunikwa na mabuu. Neno: Bibilia Takatifu Hao wote hulala mavumbini, nao mabuu huwafunika wote. Neno: Maandiko Matakatifu Hao wote hulala mavumbini, nao mabuu huwafunika wote. BIBLIA KISWAHILI Wao hulala mavumbini sawasawa, Mabuu huwafunika. |
Ikiwa nimeuita uharibifu, Wewe u baba yangu; Na kuliambia buu, Wewe u mama yangu, na dada yangu;
Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu;
Tumbo lililomzaa litamsahau; buu litamla na kuona tamu; Hatakumbukwa tena; Na udhalimu utavunjwa kama mti.
Kama kondoo wamewekwa kwenda kuzimu, Na kifo kitakuwa mchungaji wao; Watu wanyofu watawamiliki asubuhi; Miili yao itaoza, kao lao ni kuzimu.
Mambo yote yawatukia wote sawasawa; kuna tukio moja kwake mwenye haki na kwake asiye haki; kwa mtu mwema na kwa mtu mwovu; kwa mtu aliye safi na kwa mtu asiye safi; kwake yeye atoaye kafara na kwake asiyetoa kafara; kama alivyo huyo mwema ndivyo alivyo mwenye dhambi; yeye aapaye na yeye aogopaye kiapo.
Baa hilo ni katika mambo yote yanayofanyika chini ya jua, ya kuwa wote wanalo tukio moja; naam, zaidi ya hayo, mioyo ya wanadamu imejaa maovu, na wazimu umo mioyoni mwao wakati walipo hai, na baadaye huenda kwa wafu.
Fahari yako imeshushwa hadi kuzimu, Na sauti ya vinanda vyako; Funza wametandazwa chini yako, Na vidudu vinakufunika.