Yobu 20:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa hiyo mawazo yangu hunipa jawabu, Kwa ajili ya haraka niliyo nayo ndani yangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Fikira zangu zanifanya nikujibu, wala siwezi kujizuia tena. Biblia Habari Njema - BHND “Fikira zangu zanifanya nikujibu, wala siwezi kujizuia tena. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Fikira zangu zanifanya nikujibu, wala siwezi kujizuia tena. Neno: Bibilia Takatifu “Mawazo yanayonisumbua yananisukuma kujibu, kwa sababu nimehangaika sana. Neno: Maandiko Matakatifu “Mawazo yanayonisumbua yananisukuma kujibu, kwa sababu nimehangaika sana. BIBLIA KISWAHILI Kwa hiyo mawazo yangu hunipa jawabu, Kwa ajili ya haraka niliyo nayo ndani yangu. |
Mtu akijaribu kuzungumza nawe, je! Utaona ni vibaya? Lakini ni nani awezaye kujizuia asinene?
Nami nilisema kwa pupa yangu, Nimekatiliwa mbali na macho yako; Lakini ulisikia sauti ya kilio changu Wakati nilipokulilia.
Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi; Bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu.
Je! Umemwona mtu mwenye kuhamaki katika maneno? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye.
Nami nikisema, Sitamtaja, wala sitasema tena kwa jina lake; basi, ndipo moyoni mwangu kumekuwamo kama moto uwakao, uliofungwa ndani ya mifupa yangu, nami nimechoka kwa kustahimili, wala siwezi kujizuia.
Mara akaingia kwa haraka mbele ya mfalme, akaomba akisema, Nataka unipe sasa hivi katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji.
Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;