Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alichuma matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.
Yobu 20:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ingawa uovu ni mtamu kinywani mwake, Ingawa auficha chini ya ulimi wake; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Mdomoni mwake uovu ni mtamu kama sukari, anauficha chini ya ulimi wake; Biblia Habari Njema - BHND “Mdomoni mwake uovu ni mtamu kama sukari, anauficha chini ya ulimi wake; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Mdomoni mwake uovu ni mtamu kama sukari, anauficha chini ya ulimi wake; Neno: Bibilia Takatifu “Ingawa uovu ni mtamu kinywani mwake naye huuficha chini ya ulimi wake, Neno: Maandiko Matakatifu “Ingawa uovu ni mtamu kinywani mwake naye huuficha chini ya ulimi wake, BIBLIA KISWAHILI Ingawa uovu ni mtamu kinywani mwake, Ingawa auficha chini ya ulimi wake; |
Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alichuma matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.
Basi Daudi akamwambia Uria, Ngoja hapa leo tena, na kesho nitakuacha kwenda zako. Basi Uria akakaa Yerusalemu siku ile, na siku ya pili yake.
Sembuse mtu ambaye ni mwenye kuchukiza na uchafu, Mwanadamu anywaye uovu kama anywavyo maji!
Kinywa chake kimejaa laana, Na hila na dhuluma. Chini ya ulimi wake kuna madhara na uovu,
Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na kinachotamaniwa na macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.
Uovu wako mwenyewe utakurudi, maasi yako yatakukaripia; ujue, basi, ukaone, ya kuwa ni jambo baya sana na uchungu, kuwa umemwacha BWANA, Mungu wako, na ya kuwa moyoni mwako hamna kunihofu, asema Bwana, BWANA wa majeshi.