naye atamrudishia yule mwana-kondoo mara nne, kwa sababu ametenda neno hili, na kwa sababu hakuwa na huruma.
Yobu 20:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Watoto wake watataka fadhili kwa maskini, Na mikono yake itarudisha mali yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yeye mwenyewe itambidi kurudisha mali yake yote, watoto wake wataomba huruma kwa maskini. Biblia Habari Njema - BHND Yeye mwenyewe itambidi kurudisha mali yake yote, watoto wake wataomba huruma kwa maskini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yeye mwenyewe itambidi kurudisha mali yake yote, watoto wake wataomba huruma kwa maskini. Neno: Bibilia Takatifu Watoto wake watalipa yote baba yao aliyowadhulumu maskini, nayo mikono yake itarudisha mali yote aliyonyang’anya watu. Neno: Maandiko Matakatifu Watoto wake watalipa yote baba yao aliyowadhulumu maskini, nayo mikono yake itarudisha mali yote aliyonyang’anya watu. BIBLIA KISWAHILI Watoto wake watataka fadhili kwa maskini, Na mikono yake itarudisha mali yake. |
naye atamrudishia yule mwana-kondoo mara nne, kwa sababu ametenda neno hili, na kwa sababu hakuwa na huruma.
Simba mzee huangamia kwa kukosa mawindo, Nao watoto wa simba jike wametawanyika mbalimbali.
BWANA akawajalia kupendelewa na Wamisri hata wakawapa kila walichokitaka. Nao wakawateka Wamisri nyara.
Mtu akiiba ng'ombe au kondoo, na kumchinja, au kumwuza; atalipa ng'ombe watano badala ya ng'ombe mmoja, na kondoo wanne badala ya kondoo mmoja.
Lakini kama jua limekucha juu yake, ndipo patakuwa na malipizo ya damu kwa ajili yake; ingempasa kutoa malipo kamili; akiwa hana kitu, na auzwe kwa ajili ya wizi wake.
Zakayo akasimama, akamwambia Bwana, Tazama, Bwana, nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang'anya mtu kitu kwa hila namrudishia mara nne.