Naye Tamari akatia majivu kichwani mwake, akairarua hiyo kanzu ndefu yake aliyoivaa, akaweka mkono kichwani akaenda zake huku akilia kwa sauti.
Yobu 2:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naye akashika kigae cha kujikunia; akaketi majivuni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yobu akatwaa kigae, akajikuna nacho na kuketi kwenye majivu. Biblia Habari Njema - BHND Yobu akatwaa kigae, akajikuna nacho na kuketi kwenye majivu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yobu akatwaa kigae, akajikuna nacho na kuketi kwenye majivu. Neno: Bibilia Takatifu Ndipo Ayubu akachukua kigae na kujikuna nacho, huku akiketi kwenye majivu. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo Ayubu akachukua kigae na kujikuna nacho huku akiketi kwenye majivu. BIBLIA KISWAHILI Naye akashika kigae cha kujikunia; akaketi majivuni. |
Naye Tamari akatia majivu kichwani mwake, akairarua hiyo kanzu ndefu yake aliyoivaa, akaweka mkono kichwani akaenda zake huku akilia kwa sauti.
Basi Mordekai alipojua mambo yote yaliyofanyika, alizirarua nguo zake, akajivika gunia na kujipaka majivu, akatoka hadi katikati ya mji, akalia kwa sauti kuu ya uchungu.
Na katika kila mkoa, ambako amri ya mfalme na mbiu yake imewasili, palikuwako msiba mkuu kwa Wayahudi, na kufunga, na kulia, na kuomboleza; hata na wengi wakalala juu ya gunia na majivu.
Ndipo mkewe akamwambia, Je! Wewe hata sasa washikamana na utimilifu wako? Mkufuru Mungu, ufe.
kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji la maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na BWANA, ili atukuzwe.
Ee binti wa watu wangu, ujivike nguo ya magunia, na kugaagaa katika majivu; fanya maombolezo, kama maombolezo kwa ajili ya mwana wa pekee, maombolezo ya uchungu mwingi; maana mwenye kuteka nyara atakuja juu yetu ghafla.
nao wataomboleza kwa sauti juu yako, nao watalia kwa uchungu, na kutupa mavumbi juu ya vichwa vyao, na kugaagaa katika majivu;
Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu.
Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu.