Je! Ni vema kwako wewe kuonea, Na kuidharau kazi ya mikono yako, Na kuiunga mkono mipango ya waovu?
Yobu 19:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tazama, nalia, Udhalimu, lakini sisikiwi; Naulilia msaada, wala hapana hukumu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tazama napiga yowe: ‘Dhuluma!’ Lakini sijibiwi. Naita kwa sauti kubwa, lakini sipati haki yangu. Biblia Habari Njema - BHND Tazama napiga yowe: ‘Dhuluma!’ Lakini sijibiwi. Naita kwa sauti kubwa, lakini sipati haki yangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tazama napiga yowe: ‘Dhuluma!’ lakini sijibiwi. Naita kwa sauti kubwa, lakini sipati haki yangu. Neno: Bibilia Takatifu “Ingawa ninalia, ‘Nimetendewa mabaya!’ sipati jibu; ingawa ninaomba msaada, hakuna haki. Neno: Maandiko Matakatifu “Ingawa ninalia, ‘Nimetendewa mabaya!’ sipati jibu; ingawa ninaomba msaada, hakuna haki. BIBLIA KISWAHILI Tazama, nalia, Udhalimu, lakini sisikiwi; Naulilia msaada, wala hapana hukumu. |
Je! Ni vema kwako wewe kuonea, Na kuidharau kazi ya mikono yako, Na kuiunga mkono mipango ya waovu?
Dunia imetiwa mkononi mwa waovu; Yeye hufunika nyuso za waamuzi wake; Kama si yeye, ni nani basi?
Maana kila ninenapo napiga kelele, nalia, Dhuluma na uharibifu! Kwa kuwa neno la BWANA limefanywa shutumu kwangu, na dhihaka, mchana kutwa.