Wakaniambia, Watu waliosalimika, waliosalia huko katika mkoa ule, wamo katika hali ya dhiki kubwa na aibu; tena ukuta wa Yerusalemu umebomolewa, na malango yake yameteketezwa kwa moto.
Yobu 19:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ikiwa mtajitukuza juu yangu, Na kufanya aibu yangu kuwa hoja juu yangu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mnaishusha hadhi yangu mpate kujikuza; mnanilaumu kwa kunyenyekezwa kwangu. Biblia Habari Njema - BHND Mnaishusha hadhi yangu mpate kujikuza; mnanilaumu kwa kunyenyekezwa kwangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mnaishusha hadhi yangu mpate kujikuza; mnanilaumu kwa kunyenyekezwa kwangu. Neno: Bibilia Takatifu Kama kweli mngejitukuza wenyewe juu yangu, na kutumia unyonge wangu dhidi yangu, Neno: Maandiko Matakatifu Kama kweli mngejitukuza wenyewe juu yangu, na kutumia unyonge wangu dhidi yangu, BIBLIA KISWAHILI Ikiwa mtajitukuza juu yangu, Na kufanya aibu yangu kuwa hoja juu yangu; |
Wakaniambia, Watu waliosalimika, waliosalia huko katika mkoa ule, wamo katika hali ya dhiki kubwa na aibu; tena ukuta wa Yerusalemu umebomolewa, na malango yake yameteketezwa kwa moto.
Waaibishwe, wafedheheshwe pamoja, Wanaoifurahia hali yangu mbaya. Wavikwe aibu na fedheha, Wanaojikuza juu yangu.
Maana nilisema, Wasije wakanifurahia; Wale wanaojitukuza juu yangu Mguu wangu unapoteleza.
Kwa neno hili nimejua ya kuwa wapendezwa nami, Kwa kuwa adui yangu hajivunii kunishinda.
Kwa maana si adui aliyenitukana; Kama ndivyo, ningevumilia. Aliyejitukuza juu yangu siye anichukiaye; Kama ndivyo, ningejificha asinione.
Na siku hiyo wanawake saba watamshika mwanaume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu.
Usifurahi juu yangu, Ee adui yangu; niangukapo, nitasimama tena; nikaapo gizani, BWANA atakuwa nuru kwangu.
Mambo hayo yatawapata kwa sababu ya kiburi chao, kwa kuwa wamewatukana watu wa BWANA wa majeshi, na kujitukuza juu yao.
Naye BWANA ataziokoa hema za Yuda kwanza, ili utukufu wa nyumba ya Daudi, na utukufu wa wenyeji wa Yerusalemu, usipate kutukuzwa kuliko Yuda.
Hivi ndivyo alivyonitendea Bwana katika siku zile alizoniangalia ili kuniondolea aibu yangu mbele ya watu.
Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu?
Wakajibu, wakamwambia, Ama! Wewe ulizaliwa katika dhambi tupu, nawe unatufundisha sisi? Wakamtoa nje.