Akakwea kutoka huko mpaka Betheli; naye alipokuwa akienda njiani, wakatoka vijana katika mji, wakamfanyizia mzaha, wakamwambia, Paa wewe mwenye upaa! Paa wewe mwenye upaa!
Yobu 19:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hata watoto wadogo hunidharau; Nikiondoka, huninena. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hata watoto wadogo hunidharau, mara ninapojitokeza wao hunizomea. Biblia Habari Njema - BHND Hata watoto wadogo hunidharau, mara ninapojitokeza wao hunizomea. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hata watoto wadogo hunidharau, mara ninapojitokeza wao hunizomea. Neno: Bibilia Takatifu Hata watoto wadogo hunidhihaki; ninapojitokeza, hunifanyia mzaha. Neno: Maandiko Matakatifu Hata watoto wadogo hunidhihaki; ninapojitokeza, hunifanyia mzaha. BIBLIA KISWAHILI Hata watoto wadogo hunidharau; Nikiondoka, huninena. |
Akakwea kutoka huko mpaka Betheli; naye alipokuwa akienda njiani, wakatoka vijana katika mji, wakamfanyizia mzaha, wakamwambia, Paa wewe mwenye upaa! Paa wewe mwenye upaa!
Lakini sasa hao walio wadogo wangu hunifanyia mzaha, Ambao baba zao ningewadharau hata kuwasimamia mbwa wa kundi langu.
Kwa mkono wangu wa kulia huinuka kundi; Huisukuma miguu yangu kando, Na kunipandishia njia zao za uharibifu.
Nao watu wataonewa, kila mtu na mwenziwe, na kila mtu na jirani yake; mtoto atajivuna mbele ya mzee, na mtu mnyonge mbele ya mtu mwenye heshima.