Yobu 18:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wewe ujiraruaye mwenyewe katika hasira yako, Je! Dunia itaachwa kwa ajili yako wewe? Au jabali litaondolewa mahali pake? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wewe unajirarua mwenyewe kwa hasira zako. Kwani, dunia itaachwa tupu kwa ajili yako au miamba ihamishwe toka mahali pake? Biblia Habari Njema - BHND Wewe unajirarua mwenyewe kwa hasira zako. Kwani, dunia itaachwa tupu kwa ajili yako au miamba ihamishwe toka mahali pake? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wewe unajirarua mwenyewe kwa hasira zako. Kwani, dunia itaachwa tupu kwa ajili yako au miamba ihamishwe toka mahali pake? Neno: Bibilia Takatifu Wewe unayejirarua mwenyewe vipande vipande katika hasira yako, je, dunia iachwe kwa ajili yako wewe? Au ni lazima miamba iondolewe mahali pake? Neno: Maandiko Matakatifu Wewe unayejirarua mwenyewe vipande vipande katika hasira yako, je, dunia iachwe kwa ajili yako wewe? Au ni lazima miamba iondolewe mahali pake? BIBLIA KISWAHILI Wewe ujiraruaye mwenyewe katika hasira yako, Je! Dunia itaachwa kwa ajili yako wewe? Au jabali litaondolewa mahali pake? |
Amenirarua katika ghadhabu zake, na kunionea; Amesagasaga meno juu yangu; Mtesi wangu hunikazia macho makali.
Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; bali wema wangu hautaondoka kwako, wala agano langu la amani halitaondolewa; asema BWANA akurehemuye.
Ndipo akaniambia, Uovu wa nyumba ya Israeli na Yuda ni mwingi sana, nayo nchi imejaa damu, nao mji umejaa kupotosha hukumu; maana husema, BWANA ameiacha nchi hii, naye BWANA haoni.
Mungu akamwambia Yona, Je! Unatenda vema kukasirika kwa ajili ya mtango? Naye akasema, Ndiyo, natenda vema kukasirika hata kufa.
na kila ampagaapo, humbwaga chini, naye hutoka povu na kusaga meno na kukonda; nikasema na wanafunzi wako wamtoe pepo, wasiweze.
Na tazama, pepo humpagaa, naye mara hupiga kelele; tena humtia kifafa, huku anatokwa na povu, wala hamwachi ila kwa shida, akimchubua-chubua.