Yobu 18:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kumbukumbu lake litakoma katika nchi, Wala hatakuwa na jina mashambani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nchini hakuna atakayemkumbuka; jina lake halitatamkwa tena barabarani. Biblia Habari Njema - BHND Nchini hakuna atakayemkumbuka; jina lake halitatamkwa tena barabarani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nchini hakuna atakayemkumbuka; jina lake halitatamkwa tena barabarani. Neno: Bibilia Takatifu Kumbukumbu lake litatoweka katika dunia, wala hatakuwa na jina katika nchi. Neno: Maandiko Matakatifu Kumbukumbu lake litatoweka katika dunia, wala hatakuwa na jina katika nchi. BIBLIA KISWAHILI Kumbukumbu lake litakoma katika nchi, Wala hatakuwa na jina mashambani. |
Tumbo lililomzaa litamsahau; buu litamla na kuona tamu; Hatakumbukwa tena; Na udhalimu utavunjwa kama mti.
Wamesema, Njoni, tuwakatilie mbali wasiwe taifa, Na jina la Israeli halitakumbukwa tena.
Adui wameangamia na kuwa magofu milele. Nayo miji yao uliing'oa; Hata kumbukumbu lao limepotea.
Hutaungamanishwa pamoja nao katika mazishi, Kwa maana umeiharibu nchi yako, Umewaua watu wako; Kizazi chao watendao uovu hakitatajwa milele.
Wao wamekufa, hawataishi; wamekwisha kufariki, hawatafufuka; kwa sababu hiyo umewajia, na kuwaangamiza, na kuupoteza ukumbusho wao.
Tena BWANA ametoa amri katika habari zako, ya kwamba asiwepo tena mtu awaye yote mwenye jina lako; toka nyumba ya miungu yako nitakatilia mbali sanamu ya kuchora, na sanamu ya kuyeyusha; nitakufanyia kaburi lako; kwa maana u mbovu.