Yobu 18:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Utakula via vya mwili wake, Naam, mzaliwa wa kwanza wa mauti atavila via vyake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Ugonjwa mbaya unakula ngozi yake, maradhi ya kifo hula viungo vyake. Biblia Habari Njema - BHND “Ugonjwa mbaya unakula ngozi yake, maradhi ya kifo hula viungo vyake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Ugonjwa mbaya unakula ngozi yake, maradhi ya kifo hula viungo vyake. Neno: Bibilia Takatifu Nayo yatakula sehemu ya ngozi yake; mzaliwa wa kwanza wa mauti atakula maungo yake. Neno: Maandiko Matakatifu Nayo yatakula sehemu ya ngozi yake; mzaliwa wa kwanza wa mauti atakula maungo yake. BIBLIA KISWAHILI Utakula via vya mwili wake, Naam, mzaliwa wa kwanza wa mauti atavila via vyake. |
Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza, Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu.
Nao walio maskini kabisa watakula, Na wahitaji watajilaza salama; Nami nitatia shina lako kwa njaa, Na mabaki yako watauawa.
Nilishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi ambayo mapingo yake yanafunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka humo shimoni, Ee BWANA, Mungu wangu,
Na hii ndiyo tauni, ambayo BWANA atawapiga watu wote waliofanya vita juu ya Yerusalemu; nyama ya mwili wao itaharibika, wakiwa wamesimama kwa miguu yao, na macho yao yataharibika ndani ya vichwa vyao, na ndimi zao zitaharibika vinywani mwao.
Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa wanyama wa nchi.