Yobu 17:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini rudini; ninyi nyote, njoni sasa; Wala sitampata mtu mwenye hekima kati yenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini nyinyi njoni, njoni nyote tena, kwenu sitampata mwenye hekima hata mmoja. Biblia Habari Njema - BHND Lakini nyinyi njoni, njoni nyote tena, kwenu sitampata mwenye hekima hata mmoja. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini nyinyi njoni, njoni nyote tena, kwenu sitampata mwenye hekima hata mmoja. Neno: Bibilia Takatifu “Lakini ninyi njooni, ninyi nyote, jaribuni tena! Sitampata mtu mwenye hekima miongoni mwenu. Neno: Maandiko Matakatifu “Lakini ninyi njooni, ninyi nyote, jaribuni tena! Sitampata mtu mwenye hekima miongoni mwenu. BIBLIA KISWAHILI Lakini rudini; ninyi nyote, njoni sasa; Wala sitampata mtu mwenye hekima kati yenu. |
Je! Wewe wajua neno lipi, ambalo sisi hatulijui? Nawe wafahamu nini, ambalo halimo ndani yetu?
Basi ikawa, baada ya BWANA kumwambia Ayubu maneno hayo, BWANA akamwambia huyo Elifazi Mtemani, Hasira zangu zinawaka juu yako, na juu ya hao rafiki zako wawili; kwa kuwa ninyi hamkunena yaliyo sawa katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu.
Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia.
Yuko wapi mwenye hekima? Yuko wapi mwandishi? Yuko wapi mleta hoja wa nyakati hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu?
Nasema hayo nipate kuwatahayarisha. Je! Ndivyo, kwamba kwenu hakuna hata mtu mmoja mwenye hekima, awezaye kukata maneno ya ndugu zake?