Yobu 16:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Uso wangu umeharibika kwa kutoa machozi, Na giza tupu liko katika kope zangu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uso wangu ni mwekundu kwa kulia, kope zangu zimekuwa nyeusi ti; Biblia Habari Njema - BHND Uso wangu ni mwekundu kwa kulia, kope zangu zimekuwa nyeusi ti; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uso wangu ni mwekundu kwa kulia, kope zangu zimekuwa nyeusi ti; Neno: Bibilia Takatifu Uso wangu umekuwa mwekundu kwa kulia, macho yangu yamepigwa na giza. Neno: Maandiko Matakatifu Uso wangu umekuwa mwekundu kwa kulia, macho yangu yamepigwa na giza kuu. BIBLIA KISWAHILI Uso wangu umeharibika kwa kutoa machozi, Na giza tupu liko katika kope zangu; |
Jicho langu nalo limekuwa giza kwa sababu ya majonzi, Na viungo vyangu vyote vimekuwa kama kivuli.
Maana asubuhi kwao wote ni kama giza tupu; Maana wao wavijua vitisho vya hiyo giza tupu.
Ee BWANA, unifadhili, maana ni katika dhiki, Jicho langu limenyauka kwa masumbufu, Naam, mwili wangu na nafsi yangu.
Nimechoka kwa kulia kwangu, Koo yangu imekauka. Macho yangu yamedhoofika Kwa kumngoja Mungu wangu.
Kama vile wengi walivyokustaajabia, (uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu yeyote, na umbo lake zaidi ya wanadamu),
Mimi ninayalilia mambo hayo; Jicho langu, jicho langu linachuruzika machozi; Kwa kuwa mfariji yuko mbali nami, Ambaye ilimpasa kunihuisha nafsi; Watoto wangu wameachwa peke yao, Kwa sababu huyo adui ameshinda.