Yobu 16:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nimeshona nguo ya magunia juu ya mwili wangu, Na nguvu zangu nimezibwaga mavumbini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Nimejishonea mavazi ya gunia, fahari yangu nimeibwaga mavumbini. Biblia Habari Njema - BHND “Nimejishonea mavazi ya gunia, fahari yangu nimeibwaga mavumbini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Nimejishonea mavazi ya gunia, fahari yangu nimeibwaga mavumbini. Neno: Bibilia Takatifu “Nimejishonea gunia juu ya mwili wangu, nami nimezika paji la uso wangu kwenye vumbi. Neno: Maandiko Matakatifu “Nimejishonea nguo ya gunia juu ya mwili wangu nami nimekizika kipaji cha uso wangu kwenye vumbi. BIBLIA KISWAHILI Nimeshona nguo ya magunia juu ya mwili wangu, Na nguvu zangu nimezibwaga mavumbini. |
Ikawa, Ahabu alipoyasikia maneno hayo, akayararua mavazi yake, akavaa magunia mwilini mwake, akafunga, akajilaza juu ya magunia, akaenda kwa upole.
Basi adui na anifuatie, Na kuikamata nafsi yangu; Naam, aukanyage uzima wangu, Na kuulaza utukufu wangu mavumbini.
Siku hiyo Bwana, BWANA wa majeshi, akawaita watu walie na kuomboleza, na kung'oa nywele zao, na kuvaa nguo za magunia;
Naye Hana akaomba, akasema, Moyo wangu wamshangilia BWANA, Pembe yangu imetukuka katika BWANA, Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu; Kwa kuwa naufurahia wokovu wako;
Washindanao na BWANA watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; BWANA ataihukumu dunia yote; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake.