Je! Ni vema kwako wewe kuonea, Na kuidharau kazi ya mikono yako, Na kuiunga mkono mipango ya waovu?
Yobu 16:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mungu amenitia kwa hao wapotovu, Na kunitupa mikononi mwao waovu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mungu amenitia mikononi mwa wajeuri, na kunitupa mikononi mwa waovu. Biblia Habari Njema - BHND Mungu amenitia mikononi mwa wajeuri, na kunitupa mikononi mwa waovu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mungu amenitia mikononi mwa wajeuri, na kunitupa mikononi mwa waovu. Neno: Bibilia Takatifu Mungu amenigeuzia kwa watu wapotovu, na kunitupa katika makucha ya waovu. Neno: Maandiko Matakatifu Mungu amenigeuzia kwa watu wabaya, na kunitupa katika makucha ya waovu. BIBLIA KISWAHILI Mungu amenitia kwa hao wapotovu, Na kunitupa mikononi mwao waovu. |
Je! Ni vema kwako wewe kuonea, Na kuidharau kazi ya mikono yako, Na kuiunga mkono mipango ya waovu?
Wamenifumbulia vinywa vyao; Wamenipiga shavuni kwa kunitukana; Hukutana pamoja juu yangu.
Nilikuwa katika raha, naye akanivunjavunja; Naam, amenishika shingo, na kuniponda; Tena amenisimamisha niwe shabaha yake.
Basi Shetani akatoka mbele za uso wa BWANA, akampiga Ayubu na majipu mabaya tangu wayo wa mguu hadi utosi wa kichwa.
Dunia imetiwa mkononi mwa waovu; Yeye hufunika nyuso za waamuzi wake; Kama si yeye, ni nani basi?
Usinitie katika nia ya watesi wangu; Maana mashahidi wa uongo wamenijia, Nao watoao jeuri kama pumzi.
Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nilipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi.
Nawe umeonesha leo jinsi ulivyonitendea mema, kwani BWANA aliponitia mikononi mwako, hukuniua.