Yobu 15:31 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Asiutumainie ubatili, na kujidanganya; Kwa kuwa huo ubatili ndio utakaokuwa ujira wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Heri aache kutumainia upuuzi na kujidanganya, maana upuuzi ndio utakaokuwa tuzo lake. Biblia Habari Njema - BHND Heri aache kutumainia upuuzi na kujidanganya, maana upuuzi ndio utakaokuwa tuzo lake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Heri aache kutumainia upuuzi na kujidanganya, maana upuuzi ndio utakaokuwa tuzo lake. Neno: Bibilia Takatifu Asijidanganye mwenyewe kutumainia ubatili, kwa kuwa hatapata malipo yoyote. Neno: Maandiko Matakatifu Asijidanganye mwenyewe kutumainia ubatili, kwa kuwa hatapata malipo yoyote. BIBLIA KISWAHILI Asiutumainie ubatili, na kujidanganya; Kwa kuwa huo ubatili ndio utakaokuwa ujira wake. |
Msiitumainie dhuluma, Wala msijivune kwa unyang'anyi; Mali izidipo msiiangalie sana moyoni.
Hula majivu; moyo uliodanganyika umempotosha, asiweze kuiokoa nafsi yake, wala kusema, Je! Sio uongo mkononi mwangu?
Hakuna anayeshitaki kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu.
BWANA asema hivi, Msijidanganye mkisema, Bila shaka Wakaldayo watatuacha na kwenda zao; maana hawatawaacha.
Kwa maana wao hupanda upepo, nao watavuna tufani; nafaka haina bua; machipuko yake hayatoi masuke; hata ikiwa yatoa, wageni watayameza.
Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi.