Je! Ni vema kwako wewe kuonea, Na kuidharau kazi ya mikono yako, Na kuiunga mkono mipango ya waovu?
Yobu 14:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wewe ungeita, nami ningekujibu; Ungekuwa na tamaa ya kazi ya mikono yako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hapo ungeniita, nami ningeitika, wakati ungetaka kuniona mimi kiumbe chako. Biblia Habari Njema - BHND Hapo ungeniita, nami ningeitika, wakati ungetaka kuniona mimi kiumbe chako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hapo ungeniita, nami ningeitika, wakati ungetaka kuniona mimi kiumbe chako. Neno: Bibilia Takatifu Utaniita nami nitakuitika; utakionea shauku kiumbe ambacho mikono yako ilikiumba. Neno: Maandiko Matakatifu Utaniita nami nitakuitika; utakionea shauku kiumbe ambacho mikono yako ilikiumba. BIBLIA KISWAHILI Wewe ungeita, nami ningekujibu; Ungekuwa na tamaa ya kazi ya mikono yako. |
Je! Ni vema kwako wewe kuonea, Na kuidharau kazi ya mikono yako, Na kuiunga mkono mipango ya waovu?
Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena? Mimi ningengoja siku zote za huduma yangu, Hadi kufunguliwa kwangu kunifikie.
Nawe, je! Mbona hunisamehe makosa yangu, Na kuniondolea maovu yangu? Kwa kuwa sasa nitalala mavumbini; Nawe utanitafuta kwa bidii, lakini sitakuwapo.
BWANA atanitimizia malengo yake kwangu; Ee BWANA, fadhili zako ni za milele; Usiiache kazi ya mikono yako.
Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
Basi wao wateswao kwa mapenzi ya Mungu na wamwekee amana roho zao, katika kutenda mema, kama kwa Muumba mwaminifu.
Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake, ili kusudi, atakapofunuliwa, muwe na ujasiri, wala msiaibike mbele zake katika kuja kwake.