Lakini Barzilai akamjibu mfalme, Nina miaka mingapi ya kuishi, hata mimi nipande pamoja na mfalme kwenda Yerusalemu?
Yobu 14:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena? Mimi ningengoja siku zote za huduma yangu, Hadi kufunguliwa kwangu kunifikie. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Je, mtu akifa anaweza kuishi tena? Siku zangu zote za kazi ningekungoja hadi wakati wa kufunguliwa ufike. Biblia Habari Njema - BHND Je, mtu akifa anaweza kuishi tena? Siku zangu zote za kazi ningekungoja hadi wakati wa kufunguliwa ufike. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Je, mtu akifa anaweza kuishi tena? Siku zangu zote za kazi ningekungoja hadi wakati wa kufunguliwa ufike. Neno: Bibilia Takatifu Je, kama mtu akifa, aweza kuishi tena? Siku zote za kazi zangu ngumu nitangojea kufanywa upya kwangu. Neno: Maandiko Matakatifu Je, kama mtu akifa, aweza kuishi tena? Siku zote za kazi zangu ngumu nitangojea kufanywa upya kwangu. BIBLIA KISWAHILI Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena? Mimi ningengoja siku zote za huduma yangu, Hadi kufunguliwa kwangu kunifikie. |
Lakini Barzilai akamjibu mfalme, Nina miaka mingapi ya kuishi, hata mimi nipande pamoja na mfalme kwenda Yerusalemu?
Laiti ungenificha kuzimuni, Ukanilinda kwa siri, hata ghadhabu zako zitakapopita, Na kuniandikia muda ulioamriwa, na kunikumbuka!
Kwa kuwa siku zake zimeamriwa, hesabu ya miezi yake unayo wewe, Nawe umemwekea mipaka yake asiyoweza kuipita;
Hata hivyo ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe; Hao waliomwona watasema, Yuko wapi?
Kisha baada ya mambo hayo Ayubu akaishi miaka mia moja na arubaini, naye akawaona wanawe, na wana wa wanawe, hadi kizazi cha nne.
atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.
Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.