Yehu akawakusanya watu wote, akawaambia, Ahabu alimtumikia Baali kidogo; bali Yehu atamtumikia sana.
Yobu 13:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Je! Mtanena yasiyo ya haki kwa ajili ya Mungu, Na kusema kwa udanganyifu kwa ajili yake? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Je, mnadhani mwamtumikia Mungu kwa kusema uongo? Mnafikiri kusema kwa hila kunamfaa yeye? Biblia Habari Njema - BHND Je, mnadhani mwamtumikia Mungu kwa kusema uongo? Mnafikiri kusema kwa hila kunamfaa yeye? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Je, mnadhani mwamtumikia Mungu kwa kusema uongo? Mnafikiri kusema kwa hila kunamfaa yeye? Neno: Bibilia Takatifu Je, mtazungumza kwa uovu kwa niaba ya Mungu? Je, mtazungumza kwa udanganyifu kwa niaba yake? Neno: Maandiko Matakatifu Je, mtazungumza kwa uovu kwa niaba ya Mungu? Je, mtazungumza kwa udanganyifu kwa niaba yake? BIBLIA KISWAHILI Je! Mtanena yasiyo ya haki kwa ajili ya Mungu, Na kusema kwa udanganyifu kwa ajili yake? |
Yehu akawakusanya watu wote, akawaambia, Ahabu alimtumikia Baali kidogo; bali Yehu atamtumikia sana.
Kumbuka, tafadhali, ni nani aliyeangamia akiwa hana hatia? Au ni wapi hao waelekevu walikatiliwa mbali?
Watawatenga na masinagogi; naam, saa inakuja kila mtu awauaye atakapodhania ya kuwa anamfanyia Mungu ibada.
lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la Mungu na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za Mungu.