Ndipo mimi nikatuma kwake wajumbe, kusema, Hakukufanyika mambo kama hayo uyasemayo, lakini kwa moyo wako wewe mwenyewe umeyabuni.
Yobu 13:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini ninyi hubuni maneno ya uongo, Ninyi nyote ni matabibu wasiofaa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini nyinyi mnaupakaa uongo chokaa; nyinyi nyote ni waganga wasiofaa kitu. Biblia Habari Njema - BHND Lakini nyinyi mnaupakaa uongo chokaa; nyinyi nyote ni waganga wasiofaa kitu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini nyinyi mnaupakaa uongo chokaa; nyinyi nyote ni waganga wasiofaa kitu. Neno: Bibilia Takatifu Ninyi, hata hivyo, hunipakaza uongo; ninyi ni matabibu wasiofaa kitu, ninyi nyote! Neno: Maandiko Matakatifu Ninyi, hata hivyo, hunipakaza uongo; ninyi ni matabibu wasiofaa kitu, ninyi nyote! BIBLIA KISWAHILI Lakini ninyi hubuni maneno ya uongo, Ninyi nyote ni matabibu wasiofaa. |
Ndipo mimi nikatuma kwake wajumbe, kusema, Hakukufanyika mambo kama hayo uyasemayo, lakini kwa moyo wako wewe mwenyewe umeyabuni.
Ndugu zangu wametenda udanganyifu kama kijito cha maji. Mfano wa fumbi la vijito vipitavyo.
Tazama, mimi niko juu ya hao wanaotabiri ndoto za uongo, asema BWANA, na kuzisema, na kuwakosesha watu wangu kwa uongo wao, na kwa majivuno yao ya upuzi, lakini mimi sikuwatuma, wala sikuwapa amri; wala hawatawafaidia watu hawa hata kidogo, asema BWANA.
Panda uende Gileadi, ukatwae zeri, Ee binti, bikira wa Misri; unatumia dawa nyingi bure tu; hupati kupona kamwe.
Wameliponya jeraha la watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani.
Je! Hakuna marhamu katika Gileadi? Huko hakuna tabibu? Mbona, basi, haijarejea afya ya binti ya watu wangu?
Wagonjwa hamkuwatia nguvu, wala hamkuwaponya wenye maradhi, wala hamkuwafunga waliovunjika, wala hamkuwarudisha waliofukuzwa, wala hamkuwatafuta waliopotea; bali kwa nguvu na kwa ukali mmewatawala.
Efraimu alipouona ugonjwa wake, na Yuda jeraha lake, ndipo Efraimu alipokwenda kwa Ashuru, akatuma watu kwa mfalme Yarebu; lakini yeye hawezi kuwapoza, wala hatawaponya jeraha lenu.
Yesu aliposikia aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio wagonjwa; sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.
na kuvumilia mateso mengi kutoka kwa matabibu wengi, na kugharimiwa mali yake yote aliyokuwa nayo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya.