Abrahamu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu.
Yobu 13:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maneno yenu ya hekima ni mithali ya majivu, Ngome zenu ni ngome za udongo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Misemo yenu ni methali za majivu, hoja zenu ni ngome za udongo. Biblia Habari Njema - BHND Misemo yenu ni methali za majivu, hoja zenu ni ngome za udongo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Misemo yenu ni methali za majivu, hoja zenu ni ngome za udongo. Neno: Bibilia Takatifu Maneno yenu ni mithali za majivu; utetezi wenu ni ngome za udongo wa mfinyanzi. Neno: Maandiko Matakatifu Maneno yenu ni mithali za majivu; utetezi wenu ni ngome za udongo wa mfinyanzi. BIBLIA KISWAHILI Maneno yenu ya hekima ni mithali ya majivu, Ngome zenu ni ngome za udongo. |
Abrahamu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu.
BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa kiumbe hai.
Basi imekuwaje ninyi kunituliza moyo kwa utupu mtupu, Kwa kuwa katika majibu yenu unasalia uongo tu.
Je! Si zaidi sana hao wakaao katika nyumba za udongo, Ambazo misingi yao i katika mchanga, Hao wanaopondwa kama nondo!
BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu.
Wao wamekufa, hawataishi; wamekwisha kufariki, hawatafufuka; kwa sababu hiyo umewajia, na kuwaangamiza, na kuupoteza ukumbusho wao.
Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni.