Yobu 12:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Huyaongeza mataifa, na kuyaangamiza; Huyaeneza mataifa mbali, na kuyaacha. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huyakuza mataifa kisha huyaangamiza, huyafanya yapanuke kisha huyatawanya. Biblia Habari Njema - BHND Huyakuza mataifa kisha huyaangamiza, huyafanya yapanuke kisha huyatawanya. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huyakuza mataifa kisha huyaangamiza, huyafanya yapanuke kisha huyatawanya. Neno: Bibilia Takatifu Huyafanya mataifa yatukuke na kuyaangamiza; hufanya mataifa kuwa makubwa, naye huyatawanya. Neno: Maandiko Matakatifu Huyafanya mataifa yatukuke na kuyaangamiza; hufanya mataifa kuwa makubwa, naye huyatawanya. BIBLIA KISWAHILI Huyaongeza mataifa, na kuyaangamiza; Huyaeneza mataifa mbali, na kuyaacha. |
Basi Mungu akawatendea mema wale wakunga; na hao watu wakaongezeka sana, wakaendelea na kuzidi kuwa na nguvu nyingi.
Na wana wa Israeli walikuwa na uzazi sana, na kuongezeka mno, na kuzidi kuwa wengi, nao wakaendelea na kuongezeka nguvu; na ile nchi ilikuwa imejawa na wao.
Umeliongeza hilo taifa, BWANA, umeliongeza taifa; wewe umetukuzwa, umeipanua mipaka yote ya nchi hii.
Siku zijazo Yakobo atatia mizizi; Israeli atatoa maua na kuchipuka; Nao watajaza uso wa ulimwengu matunda.
Mwangalieni Abrahamu, baba yenu, na Sara, aliyewazaa; kwa maana alipokuwa mmoja tu nilimwita, nikambariki, nikamfanya kuwa wengi.
Aliye mdogo zaidi atakuwa elfu, Na mnyonge atakuwa taifa hodari; Mimi, BWANA, nitayahimiza hayo wakati wake.
Umeliongeza taifa, umezidisha furaha yao; Wanafurahi mbele zako, Kama furaha ya wakati wa mavuno, Kama watu wafurahivyo wagawanyapo nyara.
Tena kwao itasikiwa shukrani, na sauti yao wachangamkao; nami nitawazidisha, wala hawatakuwa wachache; tena nitawatukuza, wala hawatakuwa wanyonge.
Kama vile jeshi la mbinguni haliwezi kuhesabiwa, wala mchanga wa bahari kupimwa; ndivyo nitakavyoongeza wazao wa Daudi, mtumishi wangu, na Walawi wanaonihudumia.
Nitawapigia kelele, na kuwakusanya pamoja; kwa maana nimewakomboa; nao wataongezeka kama walivyokua hapo awali.
Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;