Yobu 12:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Yeye huwaondoa makuhani wakiwa wamevuliwa nguo. Na kuwapindua mashujaa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huwaacha makuhani waende uchi; na kuwaangusha wenye nguvu. Biblia Habari Njema - BHND Huwaacha makuhani waende uchi; na kuwaangusha wenye nguvu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huwaacha makuhani waende uchi; na kuwaangusha wenye nguvu. Neno: Bibilia Takatifu Huwaondoa makuhani wakiwa wametekwa nyara, na kuwaangusha waliojiimarisha muda mrefu. Neno: Maandiko Matakatifu Huwaondoa makuhani wakiwa wametekwa nyara, na kuwaangusha waliojiimarisha muda mrefu. BIBLIA KISWAHILI Yeye huwaondoa makuhani wakiwa wamevuliwa nguo. Na kuwapindua mashujaa. |
Lakini Mungu huwadumisha wenye uwezo kwa nguvu zake; Huinuka, wasiokuwa na tumaini la kuishi.
Hufa ghafla, hata usiku wa manane; Watu hutikisika na kwenda zao, Nao mashujaa huondolewa pasipo mkono wa mtu.
Haya ndiyo BWANA amwambiayo Koreshi, masihi wake, ambaye nimemshika mkono wake wa kulia, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza nguvu za wafalme; ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa.
Kisha ikawa hapo walipomletea Yoshua hao wafalme watano hapo nje, Yoshua akawaita wanaume wote wa Israeli, akawaambia majemadari wa watu wa vita waliokwenda naye, Haya, jongeeni karibu, mweke nyayo za miguu yenu katika shingo za wafalme hawa. Nao wakajongea karibu, wakatia nyayo zao katika shingo zao.
Na wafalme hao wote na nchi zao Yoshua akatwaa kwa wakati mmoja, kwa sababu yeye BWANA, Mungu wa Israeli, alipigana kwa ajili ya Israeli,
Hawa watafanya vita na Mwana-kondoo, na Mwana-kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.